© 2022 Michigan State University Board of Trustees
Public Media from Michigan State University
Play Live Radio
Next Up:
0:00
0:00
Available On Air Stations
WKAR News

'Alikuwa mtunza amani': Wazazi wa Patrick Lyoya wataka mwana wao akumbukwe zaidi ya kuwawa kwake na askari polisi

Peter Lyoya holds up a picture of his son Patrick Lyoya, 26, in his home in Lansing, Mich., on April 14. Patrick was facedown on the ground when he was fatally shot in the head by a Grand Rapids police officer this month.
Anna Nichols
/
AP
Peter Lyoya holds up a picture of his son Patrick Lyoya, 26, in his home in Lansing, Mich., on April 14. Patrick was facedown on the ground when he was fatally shot in the head by a Grand Rapids police officer this month.

This story has been translated to Swahili by Dr. Jonathan Choti. You can read the story in English here.

Ni karibu mwezi mmoja sasa tangu kuwawa kwa Patrick Lyoya.

Askari polisi wa mji wa Grand Rapids alimuua mwanaume mwenye asili ya nchi ya DRC Kongo wakati walipambana baada ya askari huyo kumsimamisha Patrick tarehe 4 mwezi wa nne. Upelelezi wa wa Idara ya Polisi ya Jimbo la Michigan bado unaendelea, na kifo hicho kimezua maandamano na vilio vipya vya haki za watu weusi (Waafrika) waliowawa na askari polisi. Lakini kwa familia ya  Lyoya, mtoto wao anazidi tukio la kutumiwa kama ishara tu. Wanataka dunia ijue ukweli kuhusu Patrick.

Petero na Dorcas Lyoya wamekuwa wakilala sakafuni katika fleti yao tangu mtoto wao awawe.

Leo, wawazi hao wameketi ukumbini mwao, wakisikiliza nyimbo za dini ya Kikristo. Wanazungukwa na picha za Patrick zilizotundikwa kutani.

Wakizungumza kupitia mtafsiri wa Kiswahili, wanasema ni mila ya Wakongo kulala sakafuni kwa kipindi cha siku arobaini (40) baada ya kifo cha mmoja wao.

"Hata yeye, sisi wote, tunapofika hapa, hatuwezi kulala kitandani, ni lazima tulale sakafuni, huo ndio utamaduni wetu," Petero na Dorcas wanaeleza.

Jamii ya Lyoya walitoka nchi ya DRC Kongo. Walihamia mji wa Lansing mnamo mwaka wa 2014 baada ya kuishi katika kambi ya wakimbizi nchini Malawi kwa miaka mingi.

Mwana wao, Patrick, aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na sita (26) alikuwa mtoto wao wa kwanza kati ya watoto wao sita. Akiwa mtoto huko DRC Kongo, Dorcas anamkumbuka Patrick kama mtoto aliyekuwa na furaha daima aliyependa kucheza mpira wa kandanda na kushinda na jamaa zake.

“Alikuwa mtunza amani kwa sababu ilipotokea kuwa marafiki zake walianza kupigana, aliwakanya akiwaambia wasipigane ila wakae kwa amani na upendo”, alisema Damaris.

Patrick alitoka kabila la Wabafuliru wa DRC Kongo. Baba yake alisema Patrick alionyesha maadaili ya watu wa kabila lao.

“Wabafuliru ni mojawapo ya makabila zaidi ya mia nne na thelatini (430) yaliko DRC Kongo. Maana ya jina 'Bafuliru' ni watu waishio kwa kushirikiana na kwa amani pamoja kila mtu na watu wote kwa jumla," alisema Petero Lyoya.

Walipotoka DRC Kongo kuepa vita, jamii ya Lyoya wanasema kwamba walipata utulivu walipohamia Marekani. Walipokuwa wakitembelea sehemu za Lansing pamoja kama jamii siku moja, Petero anasema Patrick akiwaambia kwamba alijihisi kama vile alikuwa amefika mbinguni.

“Alikuwa akitania mmoja wa jamaa zake, aliwachekesha. Alisema, 'Unaona, tulifika hapa, ilionkana kana kwamba tunamkaribia Mungu,'" alikumbuka. "Ninamaanisha, tuna amani.Kila mtu alicheka. Inaonekana kwamba tunamkaribia Mungu sasa."

Baada ya kukaa Lansing kwa miaka kadha na wazazi wake, Patrick hatimaye alihamia mji wa Grand Rapids kutafuta nafasi nzuri za kazi. Alikusudia kuweka akiba ili aweze kuwanunulia jamaa yake nyumba.

“Lakini alikuwa akipigia wazazi wake simu kuwaambia, ‘Mnajua nini, ningependa nyinyi mje hapa, ninunue nyumba, tukae pamoja. Tutaishi pamoja kwa sababu ninataka kuoa na kuwa na familia yangu binafsi, na nyinyi mtakuwa bibi na babu. Mtamtunza mtoto wangu, na mimi nitawatunza.' Huo ni moyo shupavu!" alisema Petero Lyoya. Petero alisema mwana wake alipenda kucheza dansi mpaka akawa mwalimu wa kucheza dansi.

“Aliwafundisha vijana wengi, Wakongo, wazungu, weusi jinsi ya kucheza dansi kwa ngoma za Kiafrika," alisema.

Dorcas anasema Patrick ndiye alipanga mikutano ya familia yao na alileta muziki kwa ajili ya sherehe hizo za familia.

“Majira ya kiangazi, alitutembelea karibu kila Jumamosi. Alikuja hapa. Alituchomea nyama. Alifurahia kusherehekea pamoja na familia. Alicheza dansi. Tulifurahi, tulicheka. Kwa kweli, alikuwa mtu wa kupendeza. Alipenda kuleta familia pamoja," alisema.

Patrick aliwapigia wazazi wake simu karibu kila siku, hata kwa dakika chache wakati alikuwa na mapumziko mafupi alikokuwa akifanya kazi kiwandani huko  Grand Rapids. Usiku uliotangulia kifo chake, Patrick na wazazi wake walizungumza kwa simu kupanga sherehe ya sikukuu ya kuzaliwa ya mmoja wa wadogo zake. Sherehe hiyo ilipangwa ifanyike Jumapili iliyofuata. Badala ya kusherehekea, sasa familia inashugulukia mipango ya mazishi ya Patrick.

Askari aliyemuua kwa kumpiga risasi, Christopher Schurr, amepewa likizo ya kulipwa huku idara ya polisi ya jimbo la Michigan likiendelea  na upelelezi wa kifo cha Patrick. Chama kinachomwakilisha askari huyo kinasema pambano la Patrick na askari aliyemuua lilikuwa la hatari, basi Schurr alikuwa na haki ya kujitetea.

Akifuta machozi kutoka macho yake huku akijifunuka blanketi, Dorcas alisema kuwawa kwa mtoto wake kilikiwa kitendo cha jinai.

“Hatutaki janga lililotupata limpate mzazi mwingine. Hiki kiwe kisa cha mwisho," alisema.

Dorcas Lyoya anataka askari aliyemuua Patrick ashitakiwe kotini kwa kosa la jinai.

News from WKAR will never be behind a paywall. Ever. We need your help to keep our coverage free for everyone. Please consider supporting the news you rely on with a donation today. You can support our journalism for as little as $5. Every contribution, no matter the size, propels our vital coverage. Thank you.